Wednesday, May 19, 2010

Mimba kwa wanafunzi






MIMBA KWA WANAFUNZI

NA MARY MPANDULA.

Watoto wengi wa kike wamepotea kwa kukosa malezi bora toka kwa wazazi wao nchini Tanzania.

HAKIKA ABDALA,(anayeonekana hapo kwenye picha hizi) KIJIJI CHA NYAGAO B) binti wa miaka 17, amekatiza masomo yake kidato cha kwanza katika sekonddari ya Namangale iliyopo Lindi vijijini baada ya kujiingiza katika mapenzi kwa sababu ya hali ngumu ya maisha na kukosa malezi bora kutoka kwa wazizi wake.

Hakika amesema, kwa sasa yupo tu nyumbani na ujauzito wa miezi mitano ambao amelazimika kuacha masomo ,anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mlevi wa kupindukia.

Amesema hali hii aliipata kwa kutojua nini alikuwa akikifanya kwakuwa yeye aliingia katika mahusiano kutafuta pesa ya kujikimu kimaisha.

Amefafanua kuwa, kwasababu akiwa shule muda mwingi alikuwa akikosa chakula na huduma za msingi zinazohitajika kwa mwanafunzi, jambo lililompelekea yeye kujiingiza katika mapenzi na hatimaye kujikuta akiishia kupata ujauzito ambao anaona ni mzigo kwake kwani mwanamme aliyempa mimba kaikataa.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi 300 hupata mamba kila mwaka na kati ya miaka mitano iliyopita lindi ilikuwa na wanafunzi 144 waliokatiza masomo yao sababu ya ujauzito ,Shinyanga 111 ,Dodoma 111,Mbeya 105,hali inayojidhihilisha wazi kuwa kulingana na takwimu Mkoa wa Lindi bado upo nafasi ya juu kwa wanafunzi wengi wanaokatiza masomo kwa ajili ya ujauzito.

No comments:

Post a Comment